IQNA

Madai ya kuwepo kaburi la Nabii Yahya bin Zakaria nchini Lebanon

14:51 - April 20, 2009
Habari ID: 1767490
Mtafiti na mtaalamu wa masuala ya kihistoria wa Lebanon Mussa Salman Yasin amedai baada ya utafiti wake wa hivi karibuni kwamba kaburi la Nabii Yahya bin Zakaria (as) liko kusini mwa nchi hiyo.
Mussa Salman Yasin amesema kuwa kaburi la Nabii Yahya (as) limegunduliwa katika bonde la kale linayojulikana hadi sasa kwa jina la Mar Yahya katika eneo la kaskazini mashariki mwa Tulini huko kusini mwa Lebanon.
Mtafiti huyo amesema kuwa eneo hilo linaungana na eneo la Qabrikha la kusini mwa Lebanon na kwa mujibu wa riwaya mashuhuri Nabii Yahya bin Zakaria (as) alikatwa kichwa na mfalme muovu wa Roma Herod katika eneo hilo.
Mussa Salman Yasin amesema kuwa bonde la Mar Yahya lina turathi nyingi za thamani za kihistoria na kidini na kwamba historia inaonyesha kuwa kuna zaidi ya athari 50 za Mitume wa Mwenyezi Mungu na watoto wao katika eneo hilo.
Kwa mujibu wa kisa cha Nabii Yahya bin Zakaria kilichotajwa kwenye vitabu vya kidini na kihistoria, Mtume huyo wa Mwenyezi Mungu aliuawa kwa kukatwa kichwa na mfalme wa Roma. 390215

captcha