IQNA

Kuanza mkutano wa kimataifa wa Amani na Uadilifu katika Vitabu Vitakatifu

11:40 - April 22, 2009
Habari ID: 1768395
Mkutano wa kimataifa wa Amani na Uadilifu katika Vitabu Vitakatifu na Fikra za Kifalsafa umeanza katika mji wa Nabeul nchini Tunisia.
Shirika la habari la Tunisia (TAP) limeripoti kuwa mkutano huo utakaoendelea kwa siku nne unafanyika kwa shabaha ya kuimarisha mazungumzo kati ya tamaduni na dini mbalimbali.
Malengo mengine ya mkutano huo unaosimamiwa na Wizara ya Sayansi, Utafiti na Teknolojia ya Tunisia, yametajwa kuwa ni kuimarisha amani na uadilifu na kutumia thamani za kimataifa kwa ajili ya kustawisha maelewano na watu na nchi mbalimbali.
Watafiti, wanazuoni wa kidini, wataalamu wa elimu ya wanadamu na wahadhiri wa vyuo vikuu kutoka nchi 48 za Kiislamu, Afrika na America wanajadili maudhui za amani na uadilifu katika Qur'ani, suna za Mtume (saw), haki za binadamu na historia ya amani na uadilifu katika fikra za kifalsafa. 392136

captcha