Hayo yamesemwa na mkuu wa masuala ya utamaduni katika Taasisi ya Waqfu la Jamhuri ya Kiislalmu ya Iran ambaye ameongeza kuwa kati ya mada ambazo zinapaswa kujadiliwa katika makala hizo ni kuhusu ‘Quran na Tabligh (kuhimiza utamaduni wa Qurani) .
Amesema washiriki wanaweza kutuma muhtasari wa makala zao hadi kufikia tarehe 3 June na siku ya mwisho ya kupokea makala kamili ni tarehe 10 Juni. Natija ya makala zilizochaguliwa itatangazwa tarehe 13 July na mashindano ya 26 ya kimataifa ya Quran Tukufu yatafanyika tarehe 17 July.
Idara ya mashindano ya 26 ya kimataifa ya Quran Tukufu itachapisha makala zilizoidhinishwa na waandishi watazawadiwa.
Kuhimuza utamaduni wa Quran wa kuzuia israfu na ubadhirifu katika Qur'ani ni kati ya mada nyinginezo zitakazojadiliwa katika makala hizo.
Wanaokusudia kushiriki katika uandishi makala wanaombwa kuutembelea ukurasa ufuatao wa intaneti wenye lugha za Kirabu na Kifarsi http://26qp.ir/Mehvar.aspx
396082