IQNA

Warsha maalumu kwa wahubiri na Maulamaa Lebanon

13:03 - April 29, 2009
Habari ID: 1771380
Warsha ya kutoa mafunzo maalumu kwa wahubiri na maulamaa katika uga wa usambazaji habari imefanyika nchini Lebanon.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA mjini Beirut, warsha hiyo imefanyika katika eneo la Sur na imeandaliwa na Idara ya Waqfu wa Kiislamu. Mbali na Maulamaa na wahubiri, washiriki wengine katika warsha hiyo ni pamoja na waalimu, wataalamu wa sayansi za kidini na wafanyakazi wa idara za misaada. Warsha hiyo imesimamiwa na Sheikh Mohammad Dali, Mufti wa Sur aliyemuwakilisha Sheikh Ahmad Judi, Mkuu wa Idara ya Waqfu wa Kiislamu katika eneo hilo.
Warsha hiyo imeandaliwa kwa ushirikiano wa Jumuiya ya Ustawi pamoja na Harakati ya Kijamii ya Lebnon kwa lengo la kuongeza ujuzi wa wasomi wa kidini katika fani ya upashaji habari.
Sheikh Ahmad Judi amesema warsha kama hiyo itakuwa na nafasi muhimu katika kuinua kiwango cha ujuzi wa kihabari wa wataalamu na wasomi wa kidini. 395780
captcha