IQNA

Mkutano wa Baraza la Kiislamu la Eurasia kufanyika Istanbul

10:26 - May 02, 2009
Habari ID: 1772503
Mkutano wa saba wa Baraza la Kiislamu la Eurasia unatarajiwa kufanyika mjini Istanbul, Uturuki kuanzia tarehe 12 May mwaka huu.
Wizara ya Masuala ya Kidini ya Uturuki imetangaza kuwa mkutano huo utahudhuriwa na wasomi na wanafikra wa nchi zinazozungumza Kituruki na viongozi wa nchi nyingine za Kiislamu za Asia na Ulaya.
Mkutano huo wa siku tatu utahitimisha kazi zake kwa kutoa taarifa ya mwisho kuhusu matokeo ya uvumbuzi mpya wa kidini katika masuala ya kiutamaduni ya nchi za Asia na Ulaya. 397549
captcha