IQNA

Wananchi wa Malaysia wakusanya misaada kwa ajili ya Ghaza

9:45 - May 10, 2009
Habari ID: 1776053
Wananchi wa Malaysia wametoa mchango wao kwa watu wa Ghaza katika shughuli iliyosimamiwa na Jumuiya ya Amani Palestina.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA kusini-mashariki mwa Asia, misaada hiyo ni zaidi ya dola za Kimarekani laki 382 na misaada hiyo itatatumika kwa ajili ya ujenzi mpya wa Ghaza na kuboresha maisha ya Wapalestina wanaodhulumika katika eneo hilo.
Abdullah Zabek Abdulrahman Mkuu wa Jumuiya ya Amani Palestina ya Malaysia amesema: 'Misaada iliyokusanywa itatumiwa Wapalestina kupitia Wizara ya Mambo ya Nje ya Malaysia'.
Ameelezea matumaini yake kuwa Wamalaysia wataweza kukusanya misaada zaidi kwa ajili ya Wapalestina wa Ghaza ambao walikabiliwa na hujuma ya siku 22 ya utawala haramu wa Israel. 402001

captcha