IQNA

Mfuko wa kuwaelimisha mayatima wa Palestina wazinduliwa Jordan

10:21 - May 17, 2009
Habari ID: 1779264
Mfuko wa kuwaelimisha mayatima wa Palestina katika Ukanda wa Ghaza umezinduliwa nchini Jordan.
Kwa mujibu wa gazeti la Al Dastur la Jordan, mfuko huo ambao hadi sasa una akiba ya dola milioni 10 umezinduliwa katika siku ya kwanza ya Mkutano wa Uchumi Duniani ulioanza tarehe 15 mjini Shuneh pembizoni mwa Bayari Iliyokufa.
Mfalme Abdullah wa Jordan amehutubu katika hafla ya uzinduzi wa mfuko huo na kuashiria umuhimu wa hatua hiyo kwa kusema: “Mfuko wa Mayatima wa Palestina utakuwa na jukumu la kuwasomesha watoto 1200 mayatima waliopteza wazazi wao katika hujuma ya hivi karibuni ya Israel dhidi ya Ghaza”.
Ameongeza kuwa, kwa ujumla lengo kuu la mfuko huo ni kuboresha maisha ya wanaopata masaidbu Ghaza hasa watoto. Mfuko huo wa kuwasaidia mayatima katika Ukanda wa Ghaza umezinduliwa kwa ushirikano na uwekezaji wa shirika mmoja la uhandisi la Emarati na Taasisi ya Ushirika ya Palestina. 405710
captcha