IQNA

Kongamano la kumuenzi marehemu Allamah Fadlallah lafanyika Tehran

19:46 - July 24, 2010
Habari ID: 1961492
Mkutano wa kumkumbuka na kumuenzi marehemu Allamah Muhammad Hussein Fadhlullah umefanyika katika Msikiti wa Nour mjini Tehran na kuhudhuriwa na wanazuoni, Maulama, viongozi wa ngazi za juu kitaifa na kimataifa, wanadiplomasia wa nchi za Kiislamu na familia ya Allamah Fadhlullah.
Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyed Ali Khamenei kuhusu kuaga dunia Allamah Fadhlullah umesomwa mwanzoni mwa mkutano huo ambao umesimamiwa na Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Pamoja Madhehebu ya Kiislamu. Kati ya waliohudhuria mkutano huo uliofanyika Julai 22 ni Hujjatul Islam Mohammadi Golpayegani Mkuu wa Ofisi ya Kiongozi Muadhamu, Ayatollah Jannati Katibu wa Baraza la Kulinda Katiba, Masud Zaribafan mwakilishi wa Rais Mahmoud Ahmadinejad, Ayatollah Taskhiri Katibu Mkuu Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Pamoja Madhehebu ya Kiislamu Hujjatul Islam Akhtari Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahl-ul-Bayt (AS) na Gholam Ali Haddad Adel Mkuu wa Tume ya Utamaduni katika Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu yaani bunge la Iran .
Mwana wa kiume wa Ayatullah Muhammad Hussein Fadhlullah Hujjatul Islam Walmuslimin Sayyid Ali Fadhlullah ametoa hutuba katika mkutano huo akishukuru watayarishaji wa mkutano huo na kusema Allamah Fadhlullah alikuwa akisisitiza juu ya kuiunga mkono Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kipindi chote cha maisha yake. Amesema daima Sayyid Fadhlullah alikuwa akisisitiza kuwa Iran ndio kituo kikuu cha Uislamu na watu huru kote duniani na daima alikuwa akiunga mkono mapambano ya Kiislamu huko Lebanon, Palestina na kila mambano ya kukabiliana na dhulma na ubeberu.Sayyid Ali Fadhlullah amesema baba yake yaani Allamah Fadhlullah amesisitiza katika maagizo yake ya mwisho juu ya udharura wa kulindwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na alikiwa akiamini kwamba Iran inapaswa kuwa na nguvu ndani ya nchi. Mwishoni mwa hutuba yake, Sayyid Ali Fadhlullah amewashukuru watayarishaji wa mkutano huo na kusema roho ya Allamah Muhammad Hussein Fadhlullah itaendelea kuwepo kila mahala penye harakati za kupambana na ubeberu na katika harakati za Kiislamu.
619768
captcha