Kipindi hicho kitakachorushwa hewani kutoka Makka kitawashirikisha wakuu wa vituo vya Kiislamu kutoka nchi za Asia, Marekani, Canada, Russia na nchi za Kiafrika.
Mkurugenzi wa Redio Qur'ani ya Saudi Arabia Abdullah bin Muhammad al Dousari amesema kuwa kipindi cha mwaka huu cha Usiku za Ramadhani kitajadili maudhui mbalimbali na kitawaalika wageni wengi kutoka nchi tofauti.
Al Dousari ameongeza kuwa mwaka huu pia Redio Qur'ani ya Saudia itakuwa na programu mbalimbali na mpya za kielimu, kidini, kimalezi na kijamii kwa ajili ya wasikilizaji wake. 628815