IQNA

Maonyesho ya Qur’ani Tukufu katika Kioo cha Sanaa kufanyika Qatar

15:32 - August 23, 2010
Habari ID: 1979609
Maonyesho ya Qur’ani Tukufu katika Kioo cha Sanaa yamepangwa kufanyika Alkhamisi ya wiki hii katika makao ya Jumuiya ya Wapiga Picha wa Qatar katika eneo la al Hilal mjini Doha.
Maonyesho hayo yatasimamiwa na Kitengo cha Utamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Qatar kikishirikiana na Jumuiya ya Wapiga Picha ya nchini humo.
Kazi za wasanii wa fani ya kaligrafia wa Iran akiwemo Pahlavanzadeh zitaonyeshwa katika maonyesho hayo.
Mkuu wa Kitengo cha Utamaduni cha Iran nchini Qatar Muhammad Mahdi Ahmadi amesema kuwa kazi hizo za kisanii za Pahlavanzadeh na wasanii wengine wa Iran zitaonyeshwa kwa mnasaba wa kuchaguliwa Qatar kuwa mji mkuu wa utamaduni wa ulimwengu wa Kiarabu katika mwaka huu wa 2010 na pia kwa mnasaba wa mwezi mtukufu wa Ramadhani. Kazi hizo zinajumuisha kaligrafia ya aya na sura za kitabu kitukufu cha Qur’ani.
Muhammad Mahdi Ahmadi ameongeza kuwa maonyesho hayo yatafanyika kwa uungaji mkono wa Waziri wa Utamaduni na Sanaa wa Qatar Hamad bin Abdul Aziz al Kawari.
Amesema kuwa yaonyesho hayo yataendelea kwa kipindi cha siku 8 na kwamba inatarajiwa kuwa maonyesho hayo yatakuwa hatua nzuri ya kuimarisha ushirikiano kati ya utamaduni wa Kifarsi na wa Kiarabu. 639450

captcha