Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, kongamano hilo litakalokuwa na anuani ya “Kiraa na Makari, Kuimarisha Ujuzi wa Kiislamu” litafanyika kwa usimamizi wa Chuo Kikuu cha Sultan Zeinabedin cha Malaysia.
Aidha taasisi ya Qur'ani ya mji wa Tarangau, Kituo cha Utafiti wa Qur'ani cha Tarangau na idara ya masuala ya Kiislamu ya mji huo ni kati ya taasisi zinazoshirikiana kuandaa kongamano hilo.
Kati ya masuala yatakayojadiliwa katika kongamano hilo la siku mbili ni pamoja na historia ya utafiti wa kiraa na makari, athari za kiraa ya Qur'ani Tukufu katika lugha ya Kiarabu, nafasi ya taasisi za Qur'ani katika kuhimiza kiraa ya Qur'ani, athari za kiraa katika fiqhi ya Kiislamu, uhusiano wa kiraa na tafsiri ya Qur'ani, hadithi kuhusu kiraa ya Qur'ani, kiraa kama njia ya kuwalingania watu Uislamu na sanaa ya kiraa ya Qura'ni na mafunzo ya Qur'ani katika madrasa.
641732