Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, kongamano hilo litafanyika kwa himaya ya Jumuiya ya Kielimu ya Uhusiano wa Kimataifa, Wizara ya Sayansi, Utafiti na Teknolojia, Wizara ya Mambo ya Nje, Wizara ya Utamaduni na Miongozo ya Kiislamu, Chuo Kikuu cha Imam Sadiq (AS), Chuo Kikuu cha Allamah Tabatabai, Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Azad Kitengo cha Rasht na Mkuu wa Mkoa wa Gilan.
Kongamano hilo linatazamiwa kujadili masuala kama vile mielekeo ya siasa za kimataifa, fiqhi ya Kiislamu na siasa za kimataifa, Uislamu na siasa na muundo wa kimataifa, mustakbali wa harakati za Kiislamu katika mfumo wa Kimataifa n.k.
651242