IQNA

Mchora-vikatuni vya kuudhalilisha Uislamu atunukiwa zawadi ya uhuru wa kusema

12:00 - September 09, 2010
Habari ID: 1991013
Kurt Westergaard, mchora-vikatuni vya kudhalilisha Uislamu na Mtume Mtukufu (saw) raia wa Denmark, jana Jumatano alitunukiwa zawadi ya uhuru wa kusema na kujieleza na serikali ya Ujerumani.
Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP Westergaard aliye na umri wa miaka 75 ametunukiwa zawadi hiyo na viongozi wa serikali ya Ujerumani kutokana na kile walichokitaja kuwa ni juhudi zake zisizochoka za kupigania uhuru wa magazeti na fikra na vilevile ushujaa wake katika kutetea thamani za demokrasia.
Westergaar ametunukiwa zawadi hiyo na Kansela Angela Merkel wa Ujerumani pamoja na viongozi wengine wa ngazi za juu wa nchi hiyo katika kikao cha kimataifa cha vyombo vya habari huko mjini Berlin, ambapo wawakilishi wa vyombo mbalimbali vya habari vya kimataifa pia wamehudhuria.
Mchoraji katuni huyo ametunukiwa zawadi hiyo eti ya eti uhuru wa kusema nchini Ujerumani katika hali ambayo waandishi habari wa nchi hiyo wanailalamikia vikali serikali ya nchi hiyo kwa kuwanyima uhuru wa kusema na kuandika kuhusiana na madai ya kutokea mauaji ya umati dhidi ya Mayahudi mashuhuri kwa jina la holocaust, katika Vita vya Pili vya Dunia. Waandishi wengi wa nchi hiyo na wa nchi nyingine za Magharibi wameteswa na kufungwa jela kwa kutaka kuchunguza au hata kuzungumzia tu suala hilo kwa mtazamo wa kielimu.
Kupewa zawadi hiyo mchorakatuni huyo mwenye chuki na dharau dhidi ya Uislamu, kunaweza pia kuharibu uhusiano wa jamii na jumuiya za Waislamu wa Ujerumani na serikali ya Berlin kwa sababu jumuiya hizo zimekuwa zikifanya vikao mbalimbali na serikali kwa madhumuni ya kutatua na kuondoa matatizo ya Waislamu, jambo ambalo limepelekea kuishi kwa amani jamii ya Waislamu na raia wengine wa nchi hiyo.
Itakumbukwa kwamba mwezi Septemba 2005 gazeti la Jyllands-Posten la Denmark lilichapisha vikatuni 12 vya Westergaar kwa kisingizio cha kushajiisha uhuru wa kusema, jambo ambalo liliakisiwa na magazeti mengine ya nchi za Ulaya kwa kisingizio hicho hicho eti cha kueteta uhuru wa kusema na kujieleza, na hivyo kuamsha hasira kubwa ya Waislamu katika pembe mbalimbali za dunia. 651223
captcha