Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA kongamano hilo litafanyika katika mji mkuu wa Bahrain Manama na linahesabiwa kuwa kongamano kubwa zaidi la kiuchumu katika eneo la Guba la Uajemi. Kongamano hilo linatazamiwa kujadili mkakati wa siku za usoni wa mfumo wa benki za Kiislamu.
Kongamano hilo litaangazia vigezo vipya vya maendeleo ambavyo vinaweza kudhamini ufanisi wa benki za Kiislamu na taasisi za uwekezaji wa Kiislamu.
Kongamano la Kimataifa la Benki za Kiislamu hufanyika kila mwaka nchini Bahrain na kuwashirikisha wataalamu na weledi wa uchumu kutoka nchi mbalimbali duniani.
651676