Makanisa hayo yametangaza kuwa yanapinga kikamilifu matamshi hayo ya kustaajabisha na yanayovunjia heshima Qur'ani Tukufu.
Andry Zaki ambaye ni naibu mkuu wa Wakristo wa Kianglikana wa Misri amesema kila mtu anayefanya makosa anapasa kuomba radhi sawa awe msomi wa kidini au mwanasiasa.
Ameongeza kuwa kuomba msamaha pekee hakutoshi bali kasisi huyo analazimika kusahihisha matamshi yake.
Katika upande mwingine Askofu wa kanisa Katoliki la Misri Antonios Aziz ameunga mkono maneno ya Andry Zaki na kusema kuwa kanisa hilo linaheshimu Waislamu na matukufu yao na linapinga mjadala wa aina yoyote unaovuruga uhusiano kati ya wafuasi wa duni na tamaduni mbalimbali nchini Misri. 663679