IQNA

Takwa kwa mahakama ya ICC iwahukumu Wazayuni

11:40 - September 30, 2010
Habari ID: 2004434
Desmond de Silva, mtaalamu wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa ameitaka Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC iliyo na makao yake huko The Hague kufuatilia kisheria hujuma ya umwagaji damu iliyotekelezwa na jeshi la utawala wa Kizayuni dhidi ya msafara wa kimataifa wa meli za misaada ya kibinadamu kwa watu wanaozingirwa na utawala huo katika Ukanda wa Gaza.
Kwa mujibu wa gazeti la Uturuki la Zaman, mwanasheria huyo wa Uingereza amesema, licha ya kuwa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa halijatoa ombi lolote rasmi la kufikishwa faili la hujuma hiyo katika Mahakama ya Kimataiha ya Jinai lakini ni wazi kuwa faili hilo linaweza kuwasilishwa kwenye mahakama hiyo hata bila kuwepo ombi kama hilo.
Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa limewataka wataalamu wake watatu wafuatilie kwa karibu hujuma hiyo na kuwaarifisha wahusika halisi waliotoa amri ya kushambuliwa kijeshi meli hizo za misaada ya kimataifa.
Tarehe 31 mwezi Mei, makomandoo wa jeshi la utawala haramu wa Israel walivamia msafara wa meli hizo za misaada ya kibinadana kwa watu wanaozingirwa wa Ukanda wa Gaza na kuwaua wanaharakati 9 wa amani raia wa Uturuki. 665409
captcha