Mashindano hayo ambayo yameandaliwa na Taasisi ya Qur'ani ya al-Iraqiyyah yamepangwa kufanyika mwishoni mwa mwezi huu wa Oktoba. Rafi' al-Aamiri, Mkuu wa taasisi hiyo iliyo na makao makuu yake mjini Kadhimein amesema kuhusu suala hilo kwamba, wanawake walio na hamu ya kushiriki kwenye mashindano hayo wanaweza kufika kwenye makao hayo na kusajili majina yao kuanzia saa tisa hadi kumi na mbili jioni kwa wakati wa Iraq.
Amesema mtihani wa utangulizi utafanyiwa watu watakaosajili majina yao na kwamba iwapo watapata alama zinazohitajika, wataruhusiwa kushiriki katika hatua ya pili na ya mwisho ya mashindano hayo. 666484