Majlisi hiyo ya maombolezo itaanza Jumanne ijayo saa moja kamili kwa wakati wa Austria.
Mashia na wafuasi wa maimamu kutoka katika kizazi cha Mtume Muhammad (saw) watahudhuria majlisi hiyo itakayokuwa na ratiba mbalimbali.
Shughuli kama hiyo ya kumkumbuka Imam Ja'far Swadiq inaanza leo katika Kituo cha Kiislamu mjini London Uingereza. Majlisi hiyo itahutubiwa na Sheikh Ahmad Hanif kutoka Canada.
Imam Ja'far Swadiq (as) ambaye ni miongoni mwa maimamu watoharifu kutoka katika kizazi cha Mtume Muhamamd (saw) aliuawa shahidi tarehe 25 Shawwal mwaka 148 Hijria katika mji mtakatifu wa Madina. 666947