IQNA

Chuo Kikuu cha Taiba Saudi Arabia chaanzisha kitengo cha kiraa za Qur'ani

15:28 - October 11, 2010
Habari ID: 2010795
Mkurugenzi wa Chuo Kikuu cha Taiba katika mji mtakatifu wa Madina amesema kuwa chuo hicho kimefungua kitengo cha kiraa za Qur'ani Tukufu.
Gazeti la al Madina limemnukuu Mansur bin Muhammad akisema kuwa kitengo hicho ni katika jitihada za kutoa umuhimu kwa taaluma ya Qur'ani.
Amesema kuwa lengo la kuanzishwa kitengo hicho cha kiraa za Qur'ani ni kutoa huduma kwa kitabu hicho, kutilia maanani kiraa kumi mashuhuri na kubainisha uhusiano kati ya kiraa hizo na taaluma nyingine za Qur'ani, elimu ya fiqhi, lugha na kadhalika.
Mansur Muhammad ameongeza kuwa Chuo Kikuu cha Taiba kina nia ya kutayarisha mazingira mazuri kwa wahakiki wa masuala ya Qur'ani kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa kisayansi na kupanua kiraa na taaluma za kitabu hicho kitukufu. Amesisitiza kuwa kufunguliwa kitengo hicho ni hatua muhimu katika uwanja wa elimu na hifdhi ya Qur'ani na kubainisha maarifa ya kitabu hicho kwa kutumia mbinu za kisasa. 672527

captcha