Kituo cha upashaji habari cha Resaonline kimeripoti kuwa kongamano hilo limetayarishwa na kanisa la First United Methodist la Illinois nchini Marekani ili kujibu madharau ya kasisi Terry Jones dhidi ya kitabu cha Mwenyezi Mungu Qu’ani Tukufu.
Kasisi mmoja wa kanisa hilo amesema kuwa kongamano hilo litahudhuriwa na viongozi wa Kiislamu na Kikristo na kutatolewa maswali na majibu kuhusu sheria za Kiislamu.
Kasisi huyo ameongeza kuwa kanisa la First United Methodist limaenzisha mpango uliopewa jina la “Usichome Qur’ani, Soma Kitabu Hicho” kwa shabaha ya kutambua vyema mafundisho ya dini ya Kiislamu na kujibu kitendo cha kuchomwa moto Qur’ani nchini Marekani. Amesema kuwa mpango huo utawahamasisha wakazi wa jimbo la Illinois kuoma na kuelewa Qur’ani.
Kasisi Deb Stanly amesema kuwa hadi sasa makumi ya nakala za tarjumi ya lugha ya Kiimgereza za Qur’ani Tukufu zimetolewa kwa wakazi wa jimbo hilo.
Kamasisi wa kanisa la First United Methodist la Illinois wamesema kuwa mwanzoni mwa mwaka ujao watawaalika maulama wa Kiislamu kuwahutubia wasiokuwa Waislamu na kutoa maelezo zaidi kuhusu dini hiyo. 675365