Programu hiyo inaonyeshwa katika chumba cha shirika la 'Pishgamane Muoj' kitengo cha programu za simu za mkononi.
Programu hiyo inaweza kusoma kiraa sita za tartili za wasomaji mashuhuri wa Qur'ani, kutarjumi Qur'ani kwa sauti na maandishi, tartumi 28 za Qur'ani za lugha ya Kifarsi, tarjumi za Qur'ani kwa lugha 12 hai duniani, tafsiri 8 za Qur'ani kwa lugha ya Kifarsi na kadhalika.
Programu hiyo iliyopewa jina la 'Hablul Matin' imeandikwa kwa hati za Othman Taha na ina kamusi ya Qur'ani Tukufu. Programu hiyo pia inamuwezesha mtumiaji kutafuta neno au maana anayotaka katika tarjumi au tafsiri ya Qur'ani, kukariri kiraa ya aya au sura makhsusi, kutuma au kuhifadhi sehemu makhsusi iliyochaguliwa na mtumiaji kupitia ujumbe mfupi au barua pepe na kadhalika. 676083