Uongozi wa Nilesat umetangaza kuwa vipindi cha televisheni ya al Safa vimesimamishwa kwa sababu ya kuwavunjia heshima Waislamu wa madhehebu ya Shia, kuzusha urongo dhidi ya madhehebu hiyo na kufanya njama za kuzusha hitilafu kati ya Shia na Suni.
Wizara ya Habari ya Misri imetangaza kuwa baada ya kuchunguza vipindi na matangazo ya televisheni ya al Safa, uongozi wa satalaiti ya Nilesat umekuta kwamba matangazo yake yanakiuka masharti ya mkataba wa pande mbili na kwa misngi huo umesimamisha matangazo yake.
Kanali ya televisheni ya al Safa inamilikiwa na Mawahabi wa Kuwait na imekuwa ikiendesha propaganda chafu za kuzusha hitilafu na fitina kati ya Waislamu na kuhujumu madhehebu ya Shia. 676053