IQNA

Washindi wa mashindano ya Qur'ani Benin wazawadiwa

10:04 - October 21, 2010
Habari ID: 2016862
Washindi wa mashindano ya kuhifadhi Qur'ani Tukufu nchini Benin magharibi mwa Afrika wametunukiwa zawadi.
Kwa mujibu wa tovuti ya Jumuiya ya Kimataifa ya Kuhifadhi Qur'ani, mashindano hayo ambayo yalifanyika kwa himaya ya jumuiya hiyo yalikuwa na washiriki 40 na yalijumuisha wanawake na wanaume.
Washiriki walishindana katika kuhifadhi Qur'ani nzima, na kutunukiwa zawadi katika sherehe zilizofanyika tarehe 19 Oktoba.
Kati ya walioshiriki katika hafla hiyo ni Imamu wa Msikiti Mkuu wa Togo Sheikh Yahya Idriss, Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu wa Benin Sheikh Mohammad Bashir Jibril, Mwakilishi wa al Azhar Sheikh Khalid Kamal, Mkuu wa Umoja wa Jumuiya za Kiislamu za Benin Sheikh Ahmad Tijani Haroun na Mwakilishi wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kuhifadhi Qur'ani Tukufu Sheikh Abdul Naim Bin Ali al Alyan.
679340

captcha