IQNA

Awamu ya mwisho ya mashindano ya kimataifa ya Qur'ani ya Russia yaanza leo

17:21 - October 24, 2010
Habari ID: 2018827
Awamu ya mwisho ya mashindano ya kimataifa ya kusoma Qur'ani ya Russia imeanza leo mjini Moscow.
Mashindano hayo ya Qur'ani yanasimamiwa na Mufti wa Russia Rawi Ainuddin na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiislamu Ekmeleddin Ihsanoglu.
Awamu ya awali ya mashindano hayo ambayo ilifanyika jana iliwashirikisha wasomaji 26 kutoka nchi mbalimbali dunia akiwemo kari wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Washindi katika awamu hiyo wamefanikiwa kuingia duru ya mwisho ambayo imeanza leo.
Mwenyekiti wa kamati inayosimamia mashindano ya kusoma Qur'ani ya Russia amesema kuwa mashindano hayo yanapewa umuhimu mkubwa katika jamii ya Russia na hayana kifani katika bara la Ulaya.
Kandokando ya mashindano hayo kunafanyika maonyesho ya kazi za kisanii ikiwa ni pamoja na ratiba ya uimbaji wa kasida wa kundi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Mashindano ya kusoma Qur'ani ya Russia yamekuwa yakifanyika kwa miongo kadhaa sasa. 681011
captcha