IQNA

Waislamu Russia waelekea Makka kwa ajili ya hija

10:08 - October 26, 2010
Habari ID: 2019699
Mamia ya Waislamu wa Russia wameanza kuwasilia nchini Saudi Arabia kwa lengo la kutekeleza ibada ya hija.
Kwa mujibu wa Sauti ya Russia, baadhi ya mahujaji wanatumia anga huku wengine wakipendelea njia ya ardhini kuelekea katika safari ya kimaanawi ya hija. Inatazamiwa kuwa Waislamu 20,500 wa Russia watashiriki katika Ibada ya hija ya mwaka huu.
Kama ilivyokuwa miaka ya huko nyuma, aghalabu ya mahujaji wa Russia ni kutoka eneo la mashariki mwa nchi hiyo na Jamhuri ya Dagestan.
682209
captcha