Kwa mujibu wa tovuti ya Lansing State Journal uamuzi wa kuandaliwa kikao hicho ulichukuliwa baada ya viongozi wa chuo kikuu hicho kupata Qur'ani iliyokuwa imechomwa moto mnamo tarehe 11 Septemba ikiwa imetupwa karibu na kituo kimoja cha Kiislamu katika mtaa wa South Harrison Lansing Mashariki.
Wanafikra na wasomi wa dini za mbinguni za Uislamu, Ukristo na Uyahudi watashiriki katika kikao hicho kilichondaliwa na kitengo cha utafiti wa Uislamu cha Chuo Kikuu cha Michigan.
Mambo yanayozusha utata na tofauti kati ya dini hizo tatu za mbinguni ni suala jingine litakalopewa uzito katika kikao hicho. 683842