IQNA

Waliokebehi vitabu vitakatifu watiwa nguvuni nchini Uswisi

13:42 - November 07, 2010
Habari ID: 2027139
Raia watatu wa Uswisi waliokuwa na nia ya kuchoma moto nakala za vitabu vya Qur'ani Tukufu na Injili wametiwa nguvuni na polisi ya nchi hiyo.
Kituo cha habari cha Dunyabulteni kimeripoti kuwa raia watatu wa Uswisi waliokuwa na nakala za Qur'ani Tukufu na Injili wamekwenda kwenye jengo la serikali mjini Bern wakiwa na nia ya kuchoma moto vitabu hivyo vitakatifu kwa wafuasi wa dini za Kiislamu na Kikristo. Hata hivyo polisi ya Uswisi iliingilia kati na kuzuia kitendo hicho kiovu.
Raia hao watatu watafikishwa mahakamani kujibu mashtaka ya kufanya uchochezi katika fikra za umma, kufanya jitihada za kueneza fikra za kibaguzi na kuvunjia heshima matukufu ya dini nyingine.
Wataalamu wa masuala ya sheria wanasema kuwa watu hao watatu huenda wakahukumiwa adhabu ya kifungo cha miaka mitatu jela iwapo watapatikana na hatia.
Kuchoma moto Qur'ani Tukufu kunaelekea kuwa mtindo sasa kati ya watu wanaohujumu dini ya Tukufu ya Kiislamu tangu baada ya kasisi muovu wa Marekani Terry Jones kutishia kukichoma moto kitabu hicho cha Mwenyezi Mungu tarehe 11 Septemba mwaka huu. 690326
captcha