Kwa mujibu wa tovuti ya Jumuiya ya Kimataifa ya Kuhifadhi Qur'ani Tukufu, hafla hiyo imefanyika Jumanne tarehe 10 Novemba katika mji wa Nairobi. Mashindano ya Kitaifa ya Kuhifadhi Qur'ani nchini Kenya yalifanyika kwa ushurikiano wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kuhifadhi Qur'ani Tukufu na Chuo cha Qur'ani Tukufu. Mashindano hayo yaliwashirikisha wanachuo 177 wa kiume na kike.
Mashindano hayo yalikuwa na viwango vitano vya kuhifadhi Qur'ani kamili maalumu kwa wenye umri wa miaka 17, kuhifadhi Qur'ani kamili kwa wenye umri wa miaka 10 na vilevile kuhifadhi Juzuu 20, Juzuu 15 na Juzuu 5 za Qur'ani Tukufu.
Sherehe za kuzawadiwa washindi hao zilihuduriwa na Badru din Abdullah wa Ubalozi wa Sudan nchini Kenya, Sheikh Mohammad Othman wa Baraza la Maulamaa Kenya na Abu Bakr Sanaan mwakilishi wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kuhifadhi Qur'ani Tukufu. 692847