IQNA

Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran: Umoja wa Kiislamu ni muhimu

9:30 - November 27, 2010
Habari ID: 2037684
Khatibu wa swala ya Ijumaa mjini Tehran Ayatullah Muhammad Emami Kashani ametoa wito wa umoja na mshikamano baina ya Waislamu kote ulimwenguni ili waweze kuvishinda vita vinavyofanywa dhidi yao na maadui wa dini hiyo tukufu.
Akirejelea ujumbe wa kihistoria kuhusu tukio la Ghadir Khum ambalo amekumbusha kuwa linakubaliwa na madhehebu ya Kishia na Kisuni, Ayatullah Kashani amewataka Waislamu duniani kujenga msingi wa mshikamano ambao utakuwa ngao ya kujilinda dhidi ya uadui na uhasama unaofanywa na maadui wa Uislamu.
Khatibu wa swala ya Ijumaa wa mjini Tehran ameashiria umuhimu wa kupatikana umoja katika ulimwengu wa Kiislamu ili kukomesha uadui na mizozo inayochochewa na Magharibi katika nchi za Iraq, Afghanistan, Lebanon na Palestina na kongeza kuwa, kumtegemea Allah, kutekeleza wajibu na kusimamia haki na ukweli ndiko kutakakoufanya ulimwengu wa Kiislamu kupiga hatua na kufaulu katika vita hivyo dhidi ya maadui wake.
Aidha, Ayatullah Kashani amelipongeza Jeshi la Kujitolea la Basiji la Iran kwa kujitolea muhanga na kuhakikisha Mapinduzi ya Kiislamu hayayumbi.
701627
captcha