IQNA

Benki kubwa zaidi ya Kiislamu duniani kuanzishwa

16:41 - November 29, 2010
Habari ID: 2039715
Shirika la Huduma za Benki la Al Baraka limesema litaanzisha benki kubwa zaidi ya Kiislamu duniani kabla ya kumalizika mwaka 2010 ambapo hisa zenye thamani ya dola bilioni tatu zitauzwa kwa umma.
Mkurugenzi wa Shirika la Huduma za Benki la Al Baraka Adnan Yusuf amesema: 'Tayari tumeshamaliza utafiti kuhusu kuanzishwa benki hii'.
Amesema benki hiyo kubwa itakuwa na mtaji wa awali wa dola bilioni 10 ambao utapatikana kupitia uuzaji hisa. Yusuf amesema wakati umewadia kuanzisha benki hiyo kwa sababu mfumo wa benki za Kiislamu unazidi kupata umashuhuri duniani. Adnan Yusuf ambaye pia ni mkurugenzi wa Umoja wa Benki za Kiarabu, amesema anatarajia benki zinginezo duniani zitafuata mfumo wa benki za Kiislamu kutokana na mafanikio ya mfumo huo katika miaka ya hivi karibuni.
Pamoja na kuwepo matatizo na mgogoro wa kiuchumi duniani, sekta ya benki za Kiislamu inaendelea kustawi kwa kasi kubwa.
703726

captcha