IQNA

Malaysia yapendekeza kufanyika mashindano ya kimataifa ya Qur'ani ya vipofu

8:21 - December 19, 2010
Habari ID: 2049238
Mke wa Waziri Mkuu wa Malaysia ametoa pendekezo la kufanyika mashindano ya kimataifa ya Qur'ani makhsusi kwa ajili ya vipofu.
Shirika rasmi la habari la Malaysia (Bernama) limeripoti kuwa Rasma Mansour ambaye alikuwa akihutubia kongamano la Kunyanyua Umma wa Kiislamu Kupitia Qur'ani, amewataka viongozi wa nchi hiyo kuanzisha mafundisho zaidi ya Qur'ani kwa kutumia hati za braili zinazotumiwa na vipofu kwa ajili ya kusoma ili idadi kubwa zaidi ya walemavu hao iweze kufaidika na mafundisho ya Qur'ani Tukufu.
Rasma Mansour amemezipongeza taasisi zisizokuwa za serikali nchini humo kwa juhudi zao kubwa za kuchapisha Qur'ani zilizoandikwa kwa hati za braili kwa kibali cha Jumuiya ya Ustawi wa Kiislamu ya Malaysia (Jakim).
Mke wa Waziri Mkuu wa Malaysia pia amewatunuku vipofu 200 misahafu iliyoandikwa kwa hati za braili.
Kongamano la Kunyanyua Umma wa Kiislamu kwa Kutumia Qur'ani limefanyika mjini Kuala Lumpur nchini Malaysia. 713814

captcha