Taarifa hiyo imesema kuwa mlipuko huo wa kigaidi hauna lengo jingine isipokuwa kutaka kuvuruga umoja na mshikamano wa taifa la Misri.
Taarifa hiyo ya al-Azhar imesema kuwa Waislamu na Wakristo wa Misri wanapasa kuwa makini na kuchukua hatua za kimantiki katika kukabiliana na makundi ya kifitina yanayojaribu kuchochea mifarakano na unafiki miongoni mwa Wamisri.
Ali Jumua, Mufti wa Misri pia amelaani kitendo hicho na kuwataka Wamisri wazingatie utulivu kwa lengo la kulinda umoja na mshikamano wa taifa hilo. Amebainisha masikitiko yake makubwa kutokana na kuuawa watu wasio na hatia katika mlipuko huo.
Mlipuko huo wa gari ulitokea Jumamosi asubuhi pembeni ya kanisa la al-Qiddissin, wakati waumini wa kanisa hilo walipokuwa wamekusanyika humo kusherehekea Sikukuu ya Krismasi. Wakristo na Waislamu kadhaa waliuawa kwenye mlipuko huo. 722756