Hafla hiyo ilianza kwa kisomo cha Qur'ani Tukufu na baada ya hapo Bw. Husseinpur, afisa mwandamizi wa Darul Qur'an alitoa maelezo kuhusu shughuli za kituo hicho cha Qur'ani na Olimpiadi.
Alisema kuwa, ‘tuna matumaini kuwa kiwango cha washiriki katika sayansi za Qur'ani na Hadithi pamoja na kiwango cha umaanawi katika jamii kitaongozeka kutokana na shughuli za kituo hiki cha Qur'ani ambazo pia zinajumuisha kozi za taaluma ya Qur'ani’.
Naye Hujjatul Islam Assarzadeh Mkurugenzi wa Darul Qur'an alisema kuwa Qur'ani Tukufu kama Neno la Mwenyezi Mungu, iko juu ya maneno mengine kama ambavyo maneneo ya Maimamu watoharifu kutoka Nyumba ya Mtume SAW ni ya haki.
Ameashiria hadithi ya Imam Ali AS aliposema, ‘tekeleza mafundisho ya Qur'ani na jaribu kuwatangulia wengine katika utekelzaji mafundisho ya kitabu hicho’.
725476