Kwa mujibu wa tovuti ya 20minutes.fr Rais Gul ambaye ni mwanachama wa ngazi za juu wa chama tawala cha Uadilifu na Ustawi nchini Uturuki amewatahadharisha Waislamu na kuwataka wawe macho dhidi ya makundi ya kigaidi na hasa yale yanayowaua ovyo watu na Waislamu wenzao kwa jina la Uislamu.
Rais Abdallah Gul ambaye alikuwa akizungumza siku ya Jumanne katika Bunge la Ulaya amesisistiza kwamba makundi yanayotekeleza mauaji kama hayo ya kigaidi hayafahamu lolote kuhusu Uislamu na kuongeza kuwa Waislamu wa Ulaya wanatofautiana na Waislamu wa maeneo mengine ya duniani kwa mtazamo wa asilia yao ya kijiografia na utekelezaji baadhi ya masuala ya kidini. 737009