IQNA

Maombolezo ya kukumbuka tukio la kuaga dunia Mtume (saw) kufanyika Najaf

18:15 - February 01, 2011
Habari ID: 2074252
Shughuli kubwa ya kukumbuka tukio chungu la kuaga dunia Mtume Muhammad (saw) itafanyika kesho Jumatano katika mji mtakatifu wa Najaf nchini Iraq kandokando ya Haram ya Imam Ali bin Abi Twalib (sa).
Ripoti zinasema kuwa maelfu ya waombolezaji wanatembea kwa miguu wakielekea mjini Najaf kwa ajili ya kuumbuka tukio chungu la kufariki dunia Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) licha ya baridi kali.
Vilevile wananchi wa Iraq wameweka mahema kandokando ya barabara hizo ambayo yanatoa huduma za vyakula, maji, na tiba kwa maelfu ya watu wanaokwenda kuzuru kaburi la Imam Ali (as) na kuhudhuria marasimu ya maombolezo ya kifo cha Mtume Muhammad (saw).
Katika upande mwingine Idara ya Afya ya mji mtakatifu wa Najaf imeanzisha vituo zaidi ya 20 vya afya kwa ajili ya kutoa huduma kwa wanaofanya ziara mjini humo. 740391
captcha