IQNA

Wazayuni wawazuia Wapalestina kuingia katika Msikiti wa al-Aqsa

16:35 - February 06, 2011
Habari ID: 2076238
Siku ya Ijumaa askari wa utawala ghasibu wa Israel waliwazuia Wapalestina kuingia katika Msikiti wa al-Aqsa kwa kuhofia kuwa wangefanya maandamano ya kuwaunga mkono ndugu zao wa Misri wanaotaka kuun'goa madarakani utawala wa kidikteta wa Rais Husni Mubarak.
Gazeti la Saudi Arabia la Arab News limeandika kuwa Sheikh Muhammad Hussein Mufti Mkuu wa Quds na Palestina amekemea vikali hatua ya askari hao ya kuzuia maelfu ya waumini kufika kwenye msikiti huo kwa lengo la kutekeleza ibada ya swala ya Ijumaa.
Askari hao waliwaruhusu watu walio na umri wa miaka 50 na zaidi kuingia katika msikiti huo kwa ajili ya kusimamisha swala hiyo.
Askari hao wamedai kuwa walilazimika kuchukua hatua hiyo kutokana na ripoti walizopokea kwamba Wapalestina walikuwa wamepanga kufanya maandamano ya kuwaunga mkono ndugu zao wa Palestina baada ya swala hiyo. 742005
captcha