Kwa mujibu wa kapteni Mehdi Meydani Naibu Mkuu wa Kituo cha Darul Qur'an katika Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema serikali ya Saudi Arabia haikutoa visa kwa washiriki Wairani na hivyo hawajaweza kushiriki katika mashindano hayo ya Qur'ani.
Ameongeza kuwa juhudi kubwa zilifanywa na maafisa wa Iran kutatua tatizo hilo lakini hawakufanikiwa.
Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Majeshi ya Nchi za Kiislamu yalianza Machi 13 katika mji mtakatifu wa Makka na yataendelea hadi Machi 25. Nchi 16 zinashiriki katika mashindano hayo.
762479