Mkuu wa tawi la Qum la Taasisi a Viwango na Utafiti wa Kiviwanda Farshad Khoshnevisan amesema mpango huo utakamilika katika safari ijayo ya rais Ahmadinejad wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mjini Qum.
Amesema kituo hicho kinahitajia wataalamu na kuongeza kuwa kuna haka ya ushirikiano kati ya wataalamu wa masuala ya fiqhi na wenye viwanda kuhusu suala hili.
Aidha amesema kutachapisha kitabu cha "Historia ya Viwango Kkatika Uislamu na Iran". Ameongeza kuwa kwa mtazamo wa Kiislamu-Kiirani suala la kuzingatia viwango bora vya bidhaa na huduma linarudi nyuma zaidi ya miaka elfu moja katika hali ambayo nchi nyingi duniani zimeaza kuzingatia viwango katika kipindi cha karne moja iliyopita.
768506