Mashindano hayo yanafanyika ili kuwachagua washindi watakaoshiriki katika hatua ya mwisho ya mashindano hayo ambayo imepangwa kufanyika katika mwezi mtukufu wa Ramadhani. Walio na hamu ya kushiriki katika mashindano hayo wanaweza kuandikisha majina yao kupitia mtandao wa televisheni ya al-Jazeera ya watoto, mashindano ambayo kwa mara ya kwanza kabisa yanawashirikisha watoto Waislamu wa kiume na kike kutoka pembe zote za dunia. Watoto 63 tu ndio watakaochaguliwa kutoka kwenye hatua hiyo ili kushindana katika hatua ya mwisho ya mashindano hayo ambapo washindi wanne wa mwisho watapata zawadi ya kuchukua nafasi ya kwanza. 769215