IQNA

Kituo cha Qurani cha Imam Ali AS chatuoa mafunzo ya Qurani kwa mbali

10:28 - April 13, 2011
Habari ID: 2104892
Tokea kuanzishwa kwake mwaka 2000, Kituo cha Qurani cha Imam Ali AS nchini Iran kimewasaidia watu zaidi ya milioni 4 kujifundisha Qurani kwa masomo ya njia ya mbali (distance learning).
Haya ni kwa mujibu wa mwanzilishi na mkurugenzi wa sasa wa Kituo cha Qurani cha Imam Ali AS Bw. Ali Mahmudian. Akizungumza na IQNA, amesema kituo hicho kinatoa mafunzo ya Qurani katika fremu ya mpango ujulikanao kama ‘Soma Qurani Ukiwa Nyumbani’.
Kwa mujibu wa mpango huo, aina mbali mbali ya vitabu hupewa wanaojiandikisha ili kuwawezsha kusoma katika muda maalumu na kasha wanatumiwa mitihani ya kubainisha ufahamu wao wa Qurani Tukufu.
Mahmudian ameongeza kuwa mpango sawa na huo umetekelezwa katika kutoa masomo kuhusu Nahjul Balagha na Al Sahifa As-Sajadiya.
771997

captcha