IQNA

Kalamu inayosoma Qur’ani yazinduliwa Kashmir

13:41 - May 15, 2011
Habari ID: 2122415
Feroz Khan mtaalamu wa masuala ya kompyuta katika mji wa Srinagar huko Kashmir inayokaliwa na India amezindua kalamu ya kompyuta ambayo inaweza kusoma aya za Qur’ani Tukufu.
Kalamu hii ya kipekee imeanzishwa kwa lengo la kustawisha utamaduni wa kusoma Qur’ani Tukufu.
Kwa msaada wa kalamu hii, mtumiaji anaweza kufahamu njia sahihi ya kusoma Qur’ani Tukufu.
Kalamu hiyo yenye hisia zenye nguvu inaweza kusoma Qur’ani nzima ikielekezwa katika ukurasa maalumu wa Qur’ani. Kalamu hiyo pia ina tekenolojia ya kuskani na kutamka aya za Qur’ani.
Khan amesema kalamu hiyo itakuwa msaada mkubwa kwa wale wanaotaka kujifunza zaidi Qur’ani na Uislamu.
791803
captcha