IQNA

Masomo ya hifdhi ya Qura'ni kwa wanawake wa Qatar kufanyika Juni

12:29 - May 26, 2011
Habari ID: 2128766
Masomo ya hifdhi ya Qur'ani maalumu kwa wanawake wa Qatar yamepangwa kufanyika kuanzia tarehe 5 mwezi Juni katika Kituo cha Hifdhi ya Qur'ani cha Maryam bin Imran kilichoko huko mjini Doha Qatar, na kuendelea kwa muda wa miezi mitatu.
Kwa mujibu wa gazeti la nchi hiyo la as-Sharq, mbali na masomo ya hifdhi ya Qur'ani, masomo mengine maalumu ya msimu wa joto yatatolewa kwa mabinti walio na umri wa kati ya miaka 5 hadi 25. Masomo hayo maalumu yamepagwa kuanza tarehe 9 Julai hadi mwishoni mwa msimu huo.
Kituo cha Maryam bint Imran pia leo Alkhamisi kinaandaa kikao maalumu kinachozungumzia uthabiti wa itikadi za kidini katika kipindi cha mifarakano na jinsi ya kujadiliwa suala hilo katika zama hizi. 798378
captcha