IQNA

Muongozo wa Qur’ani ni kwa waadamu wote

13:48 - May 31, 2011
Habari ID: 2131576
Muongozo wa Qur’ani Tukufu ni kwa ajili ya wanaadamu wote na hili linabainika katika sura ya kwanza ya Qur’ani , Fatiha, ambapo imetumika ibara ya ‘Rabbul Alameen’ na si ‘Rabbul Muslimeen’, amesema jaji wa zamani wa India.
Jaji J.S Verma ameyasema hayo katika semina ya ‘Utumiaji wa Sheria za Kiislamu katika dunia ya sasa’. Semina hiyo imetayarishwa na Akademia ya Fiqhi ya India.
Aidha ametoa wito kwa academia hiyo ya fiqhi kustawisha ufahamu bora kuhusu Uislamu na sheria za Kiislamu ili kuleta maelewano, uadilifu na usawa nchini India.
Akizungumza katika hafla hiyo Maulana Khalid Saifullah Rahmani, Katibu Mkuu wa Akademia ya Fiqhi ya India ameelezea mantiki ya sheria mbalimbali za Kiislamu kuhusu masuala ya Sheria za Kiislamu za Familia.
801582
captcha