Masomo ya kufunza mbinu za kufundisha Qur'ani Tukufu na uendeshaji wa madarasa ya Qur'ani yanaendelea nchini Bahrain kwa udhamini wa Idara ya Masuala ya Kidini ya Wizara ya Sheria, Wakfu na Masuala ya Kisilamu ya Bahrain.
Masomo hayo ambayo yalianza tarehe Saba Juni yataendelea hadi tarehe 26 Juni na yanawashirikisha walimu wa kike na kiume wa masomo ya Qur'ani.
Katika masomo hayo wakufunzi mashuhuri wa Qur'ani watatoa mafunzo maalumu kuhusu njia na mbinu za kuhifadhi na kusoma Qur'ani Tukufu kwa washiriki wa masomo hayo.
Wizara ya Sheria, Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya Bahrain imeandaa masomo hayo kwa madhumuni ya kunyanyua kiwango cha mafundisho ya Qur'ani yanayotolewa katika shule na vituo vya Qur'ani katika pembe zote za nchi hiyo. 811698