Katika uchaguzi uliofanyika Julai 18, baraza hilo lenye wanachama 35 kutoka madhehebu mbalimbali ya Kiislamu lilimchagua kiongozi mpya baada ya muhula wa Sheikh Bubakar Kulibali kumalizika.
Mwenyekiti mpya wa baraza hilo amesema: “Mikutano yetu ni fursa ya kujadili masuala ya Kiislamu na matatizo ya jamii ya Kiislamu. Hii ni katika hali ambayo tunafungamana na kufanya kila tuwezalo kuimarisha umoja wa Waislamu na kujiepusha na mifarakano ya kidini”.
Amesema baraza hilo litazingatia zaidi suala la madrasa za Qur’ani na kuandaa mipango ya kuwasaidia wanafunzi wanaohitimu kutoka madrasa hizo.
827639