IQNA

Maonyesho ya Qur’ani yaibua ‘wimbi la Qur’ani Iran’

23:35 - July 31, 2011
Habari ID: 2162810
Maonyesho ya Kimataifa ya Qur’ani ya Iran ambayo hufanyika kila mwaka mjini Tehran huibua wimbi na harakati kubwa ya Qur’ani nchini.
Hayo ni kwa mujibu wa Masood Nikdast, karii maarufu wa Qur’ani nchini Iran ambaye ameongeza kuwa maonyesho hayo ni tukio kubwa ambalo huwalkutanisha pamoja wasomi na wanaharakati wa Qur’ani kitaifa na kimataifa.
Amepongeza mafanikio yaliyopatikana hapa nchini katika uga wa Qur’ani ambayo yamewasilishwa katika maonyesho hayo na kusema taasisi zaidi za Qur’ani nchini zihusishwe. Amesema kuna vipawa tele vya Qur’ani katika miji mbalimbali ya Iran.
830749
captcha