IQNA

Kozi za Qur’ani na tarjumi ya Kiingereza katika maonyesho ya Qur’ani Tehran

15:34 - August 04, 2011
Habari ID: 2165050
Taasisi ya Qur’ani ya kutoa mfunzo ya lugha “Besharat” imeanzisha kozi kadhaa za waalimu kuhusu lugha ya Qur’ani yenye tarjumi ya Kiingereza katika Maonyesho ya Kimataifa ya Qur’ani mjini Tehran.
Kozi hiyo inajumuisha mafunzo kuhusu lugha ya Qur’ani, tadaburi juu ya aya za Qur’ani, Nahjul Balagha, mbinu za kufundisha, nahau ya Kiarabu na kufunza Qur’ani Tukufu kwa Kiingereza.
Wale watakaohudhuria kozi hiyo na kufanikiwa watapewa vyeti.
Kozi hiyo imeandaliwa ili kutoa fursa kwa washiriki kuhifadhi Qur’ani. Kusoma aya za Qur’ani, kuimarisha ufahamu wa Qur’ani na lugha ya Kiarabu.
Maonyesho ya 19 ya Kimataifa ya Qur’ani yanaendelea katika Uwanja wa Sala wa Imam Khomeini RA mjini Tehran kila siku kuanzia saa 11 jioni hadi saa sita usiku hadi tarehe 26 Ramadhani.
836331
captcha