IQNA

Vitabu vya kidini vya Iran katika maonyesho ya vitabu Zimbabwe

15:26 - August 04, 2011
Habari ID: 2165065
Kituo cha Utamaduni cha Iran nchini Zimbabwe kimewasilisha vitabu kadhaa vya kidini, kifilosofia, kiutamaduni na sana katika Maonyesho ya Kimataifa ya Vitabu mjini Harare mwaka 2011.
Kwa mujibu wa IQNA, maonyesho hayo ambayo mwaka huu yalikuwa na kaulimbiu ya ‘Kitabu kwa ajili ya Ustawi wa Afrika” yalifunguliwa na Lazarus Dokora, Naibu Waziri wa Elimu, Michezo, Sanaa na Utamaduni Zimbabwe.
Naibu Waziri Mkuu wa Zimbabwe Arthur Mutambara alitembelea kibanda cha Iran katika siku ya pili ya maonyesho ambapo alipongeza juhudi za kiutamaduni za Iran. Karibu wahadhiri 40 wa vyuo vikuu, wanachuo na viongozi wa mashirika yasiyo ya kiserikali walijisajilisha kuwa wanachama wa Maktaba ya Kituo cha Utamaduni cha Iran katika maonyesho hayo.
836670

captcha