IQNA

Utafiti wabaini Waislamu wawili kati ya watatu Ufaransa wameripoti kukumbwa na ubaguzi wa rangi

21:00 - September 17, 2025
Habari ID: 3481246
IQNA – Waislamu wawili kati ya watatu nchini Ufaransa wanasema wamekumbwa na tabia za kibaguzi, kwa mujibu wa utafiti mpya unaoangazia ubaguzi mpana katika ajira, makazi, na huduma za umma.

Utafiti uliochapishwa Septemba 15 na Taasisi ya Maoni ya Umma ya Ufaransa (Ifop) unaonyesha kuwa asilimia 66 ya Waislamu wa Ufaransa wameripoti kukumbwa na tabia za kibaguzi.

Utafiti huo, uliofadhiliwa na Msikiti Mkuu wa Paris, unadokeza kile kinachoitwa “mfumo wa ubaguzi wa sura nyingi.”

Utafiti huo ulifanyika kati ya mwezi Agosti na Septemba 2025, ukihusisha Waislamu 1,005 wenye umri wa miaka 15 na zaidi. Kwa kulinganisha, ni asilimia 20 tu ya raia wa kawaida wa Ufaransa walioripoti uzoefu kama huo mwaka 2023, jambo linaloonyesha kuwa kiwango cha Waislamu ni zaidi ya mara tatu ya wastani wa kitaifa.

Kwa mujibu wa utafiti huo, asilimia 82 ya washiriki wanaamini kuwa chuki dhidi ya Waislamu “sasa ni jambo lililoenea nchini Ufaransa.” Matokeo hayo pia yanaonyesha kuwa ubaguzi ni mkali zaidi katika maeneo ya maisha ya kila siku yanayoathiri uwezo wa mtu kupanda kijamii.

Ajira ni kikwazo kikuu. Zaidi ya nusu ya Waislamu walioshiriki (asilimia 51) walisema walikumbwa na ubaguzi walipotafuta kazi, ikilinganishwa na asilimia 7 tu kutoka makundi mengine ya kidini. Makazi nayo yanakabiliwa na changamoto kama hizo, ambapo asilimia 46 ya Waislamu waliripoti kutendewa kwa ubaguzi, ikilinganishwa na asilimia 6 tu ya wengine.

Utafiti unaonyesha pia kuwa huduma za umma, ambapo unatarajiwa uwiano na haki,pia zimeathiriwa. Takriban asilimia 36 ya Waislamu waliripoti kubaguliwa na maafisa wa utawala, asilimia 29 kutoka kwa wahudumu wa afya, na asilimia 38 kutoka kwa walimu. Takwimu hizo pia zinaonyesha ukaguzi wa polisi kama eneo kuu la matendo ya kibaguzi, ambapo asilimia 51 waliripoti uzoefu mbaya.

Chems-eddine Hafiz, mkuu wa Msikiti Mkuu wa Paris, alisema matokeo hayo yanaonyesha kuwa “vita dhidi ya chuki dhidi ya Uislamu yaani Islamofobia” haipaswi kuonekana kama “mada ya kijamii” bali kama “jambo la usalama wa kitaifa na mshikamano wa jamhuri.”

Utafiti huo pia unaonyesha kuwa mwonekano unachangia. Kuvaa mavazi ya kidini, kuzungumza kwa lafudhi ya kipekee, au kuwa na asili ya Afrika huongeza kwa kiasi kikubwa uwezekano wa kubaguliwa, kwa makadirio ya asilimia 85.

 

3494642

captcha