Ali Zahir, mkuu wa idara ya habari ya Hizbullah, alisema katika mkutano na waandishi wa habari kuwa kaulimbiu ya maadhimisho hayo ni: “Nimeshikamana na ahadi niliyoitoa.”
Aliongeza kuwa shughuli hizo zitafanyika kuanzia Septemba 25 hadi Oktoba 12, kwa mujibu wa taarifa ya Al-Ahed News.
Miongoni mwa shughuli zilizopangwa ni kuangazia mwamba wa Al-Rawsheh ulioko pwani ya Beirut kwa picha za mashahidi hao wawili, hotuba kutoka kwa Katibu Mkuu wa Hizbullah Sheikh Naim Qassem, mikusanyiko ya umma katika saa ya kuuawa shahidi Nasrallah, usomaji wa Qur’ani, mashairi, qasida, na maonyesho ya sanaa.
Sayyid Nasrallah aliuawa shahidi mnamo Septemba 27, 2024 katika shambulio la kigaidi la anga la jeshi katili la Israel lililotokea katika kitongoji cha kusini mwa Beirut, ambapo mabomu ya kisasa yaliyotengenezwa Marekani yalitumika.
Sayyid Safieddine aliongoza Hezbollah kwa muda wa wiki moja baada ya kifo cha Nasrallah, kisha yeye na wenzake kadhaa pia kuuawa shahidi katika shambulio jingine la kigaidi la Israel lililotokea Oktoba 3, 2024 katika vitongoji vya kusini mwa Beirut.
Sayyid Safieddine alijiunga na Hizbullah mwaka 1982 na alihudumu kama mkuu wa Baraza la Utendaji la harakati hiyo kuanzia mwaka 1994 hadi alipouawa shahidi.
3494636